Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP kuongeza usambazaji chakula Ivory Coast

WFP kuongeza usambazaji chakula Ivory Coast

Shirika la chakula la Umoja wa Mataifa limesema leo kuwa litaongeza usambazaji wa chakula kwa mamia ya raia wa Ivory Coast ambao wameyakimbia makazi yao na kuingia nchi jirani ya Liberia kutokana na mkwamo wa kisiasa unaoendelea nchini humo.

Wasiwasi wa kuendelea kuongezeka kwa wakimbizi wa ndani ni mkubwa hasa kutokana na vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyoendelea kushamiri hivi sasa. Mamia ya wananchi wakihofia machafuko hayo wanalazimika kukimbilia katika maeneo ya mbali ikiwemo nchi jirani ya Liberia.

Shirika hili la chakula limesema kuwa kuna udharura wa kuongeza kasi ya usambazaji wa chakula kwa ajili ya kuwafikia wakimbizi hao ambao hata hivyo ustawi wao kwenye maeneo wanayohifadhiwa bado ni wa hali ya nchini.

 

Katika kipindi cha miezi sita ijayo, WFP inakusudia kuwasaidia jumla ya watu 125,000 ambao watapewa huduma mbalimbali ikiwemo chakula na mahitaji mengine.