Skip to main content

Hukumu dhidi ya wabakaji DRC ni ishara ya kutendeka haki:UM

Hukumu dhidi ya wabakaji DRC ni ishara ya kutendeka haki:UM

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa anayehusika na unyanyasaji wa kingono katika maeneo yaliyokumbwa na vita, amekaribisha na kupongeza hatua ya kutiwa hatia na kwa maafisa kadhaa wa jeshi waliohusika kwenye matukio ya ubakaji katika maeneo ya kaskazini wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, akisema kuwa kumbe haki inaweza kupatikana.

Wanawake wapatao 24 walikumbwa na mkasa huo uliotendeka katika eneo la jimbo la Kivu, katika kipindi cha Septemba 26 na 29 mwaka uliopita. Askari hao 11 wa jeshi la Congo ambalo hujulikana kama FARDC wanalalamikiwa kutenda jinai hizo ikiwemo pamoja na kuwateka watoto wa shule, kuleta uharibifu wa majengo na udhalilishaji wa kijinsia.

 

Wote walipatikana na hatia na kuhukumiwa kwenda jela na mahakama maalumu ya kijeshi iliyoundwa kufuatilia mkasa huo. Kwa mujibu wa Margot Wallström hukumu hiyo ni ishara njema inayoonesha kwamba kumbe juhudi za kuwabana watendaji wanaokwepa adhabu sasa zimeanza kuzaa matunda.