Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP inagawa chakula kwa watu 50,000 Moghadishu

WFP inagawa chakula kwa watu 50,000 Moghadishu

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP na washirika wake wiki hii wamezanza ugawaji wa dharura wa chakula kwa watu 50,000 mjini Moghadishu ili kukabiliana na athari za ukame uliokumba eneo kubwa la Somalia.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa WFP nchini Somalia Stefano Porretti shirika hilo na wahisani wengine wanfanya kila linalowezekana kuwalisha maelfu ya Wasomali wanaokabiliwa na njaa na hususan wanawake na watoto ambao wamelazimika kuzikimbia nyumba zao kutokana na ukame na vita.

Amesema watu hao wamebanwa kila upande na wanahitaji msaada ili kunusuru maisha yao na ya watoto wao.