Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wa mitaani wasiwe adha bali wasaidiwe:Pillay

Watoto wa mitaani wasiwe adha bali wasaidiwe:Pillay

Idadi ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani duniani sasa inakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 100 kwa mujibu wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.

Akihutubia baraza la haki za binadamu mjini Geneva kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema watoto hawa wasionekane kama ni tatizo la kijamii, bali kama binadamu wenye uwezekano wa kuchangia pakubwa kwenye jamii kama chachu ya mabadiliko.

Bi Pillay ametoa wito wa kuongezwa juhudi kuwalinda watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani akibainisha kwamba wako katika hatari ya haki zao za binadamu kukiukwa ikiwemo dhulma za ngono, ukatili, manyanyaso na usafirishaji haramu wa binadamu.

(SAUTI YA NAVI PILLAY)

Bi Pillay ameongeza kuwa ukatili dhidi ya watoto wa mitaani unaofanywa na vyombo ya sheria haukubaliki. Amesema watoto wa mitaani wanhitaji kupewa uwezo wa kuzungumzia haki zao na kuhusishwa katika mipango ya maendeleo kwa lengo la kuboresha maisha yao.