Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakenya Sita wametakiwa kufika mahakama ya ICC

Wakenya Sita wametakiwa kufika mahakama ya ICC

Wakenya sita wanaoshukiwa kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa Kenya uliozua utata 2007 wametakiwa kufika mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC mjini The Hague tarehe 07 April.

Mahakama ya ICC imewaita mahakamani Wakenya hao ambao ni pamoja na mawaziri watatu waliositishwa kazi na mkuu wa zamani wa polisi.

Mwendesha mashitaka mkuu wa ICC Luis Moreno Ocampo anawashutumu washukiwa hao sita kwa kutekeleza uhalifu dhidi ya ubinadamu ikiwemo mauaji, kuhamishwa kwa lazima, utesaji na watatu kati ya hao sita limejumuishwa kosa la ubakaji. Takribani watu 1200 waliuawa na wengine zaidi ya 500,000 kuzikimbia nyumba zao wakati wa machafuko hayo ya Kenya.