Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usawa katika elimu, sayansi na teknolojia ni daraja la ajira bora kwa wanawake

Usawa katika elimu, sayansi na teknolojia ni daraja la ajira bora kwa wanawake

Leo ni siku ya wanawake duniani ambapo miaka 100 iliyopita dunia iliadhimisha kwa mara ya kwanza siku hii ya kimataifa na mkazo ukiwa katika usawa wa kijinsia na kumwezesha mwanamke katika nyanja zote.

Leo hii kwa mujibu wa ujumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kuadhimisha siku hii hatua zimepigwa kwa kupitia uelimishaji, kuchukua hatua mbalimbali, na kubadilisha sera, lakini ameonya kuwa bado katika nchi nyingi na jamii nyingi mwanamke anachukuliwa kama raia wa daraja la pili.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni fursa sawa katika elimu, sayansi na teknolojia ni daraja la kuwawezesha wanawake kupata ajira bora. Ban amesema kwa elimu baina ya wasichana na wavulana pengo limeanza kuzibwa lakini kwa masuala mengine bado wanawake na wasichana wanaendelea kubaguliwa, kutendewa ukatili na mara nyingi na wapenzi wao au ndugu wa familia.

Wanawake wanasemaje kuhusu ukombozi wa mwanamke na elimu hadi sasa?

(SAUTI YA MWANAMKE UNAMID)