Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wapalestina zaidi ya 6000 wanashikiliwa Israel

Wapalestina zaidi ya 6000 wanashikiliwa Israel

Suala la kuachiliwa kwa wafungwa zaidi ya 6000 wa Kipalestina walioko katika jela za Israel linasalia kuwa muhimu kwa utawala wa Palestina.

Hayo yamesemwa leo mjini Vienna Austria na mwenyekiti wa kamati inayoshughulika na haki za Wapalestina Abdou Salam Diallo aliyezungumza katika siku ya mwanzo ya mkutano wa siku mbili unaojadili uharaka wa kushughulikia tatizo la wafungwa wa kisiasa wa Kipalestina walioko mahabusu na magereza za Israel.

Zaidi ya wafungwa wa kisiasa 6000 wanashikiliwa na serikali ya Israel katika mahabusu na jela zao amesema bwana Diallo akiongeza kuwa wakati watu wakitarajia katika miezi ijayo kuwepo kwa taifa la Palestina, kwa mamlaka ya Palestina ni muhimu kushughulikia suala hili la wafungwa ili kwa wakati huohuo kuweza kuwa na taiafa huru na kisha kuhakikisha wafungwa wote wanaachiliwa.