Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usawa katika mafunzo, elimu, sayansi ni muhimu kwa wanawake:UM

Usawa katika mafunzo, elimu, sayansi ni muhimu kwa wanawake:UM

Kesho Machi nane ni siku ya kimataifa ya wanawake na mwaka huu pia ni maadhimisho ya 100 tangu kuanza kusherehekewa siku hiyo.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni usawa katika elimu, mafunzo na sayansi na teknolojia, ambayo ni njia bora ya kuwapa wanawake kazi za maana. Umoja wa Mataifa umesema elimu pia inachangia pakubwa katika amani na utulivu kwa kuchagiza maisha bora na uwajibikaji katika jamii.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya siasa Somalia UNIPOS imesema kwa wanawake wa Somalia ambao kwa miongo wamekuwa ni mama wa nyumbani na walezi wa watoto na jamii ili kufanikisha kauali mbiu hii lazima kuwepo na mazingira bora na ni muhimu kuwashirikisha katika upatanishi kati ya makundi na jamii za nchi hiyo.

UNIPOS imesema jukumu la wanawake wa Somalia ni muhimu sana katika kuleta amani ya nchi hiyo ambayo haina serikali kwa zaidi ya miongo miwili sasa