WFP imetoa wito wa kuwepo fursa salama kwa watoa misaada ya kibinadamu Libya

4 Machi 2011

Shirika la mpango wa chakula duniani limetoa wito wa kuwepo na fursa salama kwa wafanyakazi wa misaada nchini Libya ili chakula kiweze kufikishwa kwa maelfu ya watu wanaohitaji msaada hususani wanawake na watoto.

Hadi sasa WFP imeshasafirisha tano 80 za biskuti zinazoongeza nguvu kwenye mpaka kati ya Libya na Tunisia kukabiliana na mahitaji ya dharura ya chakula kwa watu wanaokimbia machafuko Libya. Hata hivyo tani zingine 1182 za unga wa ngano zilizokuwa zikipelekwa Benghazi Libya bado hazijawasili kwa sababu meli ilirudishwa siku ya Alhamisi kutokana na mapigano.

Hivi sasa WFP inazindua ombi la msaada wa dola zaidi ya milioni 30 kuweza kutoa msaada wa chakula kama anavyofafanua Emilia Casella msemaji wa WFP.

(SAUTI YA EMILIA CASELLA)

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter