Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC kumchunguza Qadhafi kwa madai ya uhalifu dhidi ya ubinadamu:Ocampo

3 Machi 2011

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC inamchunguza kiongozi wa Libya Muammar Qadhafi kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu amesema mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama hiyo Luis Moreno Ocampo.

Akizungumza The Hague hii leo Ocampo amesema mahakama inajukumu la kutenda haki na itafanya hivyo, hakuna atakayekwepa mkono wa sheria. Amesema uchunguzi huo unafanyika baada ya kubaini wahusika wa madai ya uhalifu huo na watakaochunguzwa ni pamoja na watoto wa Qadhafi na mkuu wa masuala ya usalama wa Libya.

(SAUTI YA MORENO OCAMPO)

Uchunguzi huo unahusiana na ukandamizaji na vitendo visivyokubalika vilivyotekelezwa na majeshi ya usalama dhidi ya waandamanaji wanaopinga utawala wa Rais Qadhafi nchini Libya.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter