Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Marekani kuisaidia Afrika Mashariki kukabili ugaidi

Marekani kuisaidia Afrika Mashariki kukabili ugaidi

Serikali ya Marekani imejitolea kwa mara nyingine kusaidia mataifa ya Afrika Mashariki, kukabiliana na ugaidi.

Msaada wa Marekani kwa njia ya kifedha kupitia mashirika ya kijamii unalenga kuhamasisha jamii nchini Kenya na nchi jirani, kuhusu athari za tendo la ugaidi.

Balozi wa Marekani nchini Kenya Michael Ranneberger leo Jumanne amezuru mjini Mombasa Pwani ya kutoa ufadhili wa dola 90, 000, kwa shirika la Kenya Community Support Centre, ambalo limezindua mpango wa kuhamasisha vijana dhidi ya ugaidi.  Mwandishi wa habari Josephat Kioko ameandaa taarifa zaidi kutoka mjini Mombasa.

(RIPOTI YA JOSEPHAT KIOKO)