Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Athari za ubakaji kwa watoto DR Congo ni kubwa:Lake

Athari za ubakaji kwa watoto DR Congo ni kubwa:Lake

Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Athony Lake ambaye hii leo yuko Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kukutana na waathirika wa ubakaji amesema athari zake kwa watoto wa nchi hiyo ni kubwa.

Amesema ubakaji unaathari za kimwili na kisaikolojia kwa watoto waliotokana na ukatili huo na haziwezi kukadiriwa. Ameongeza kuwa ubakaji unaathiri maendeleo ya jamii, unachochea machafuko ambayo ni adui wa amani na maendeleo.

Amesema juhudi za pamoja zinahitajika kuwalinda watoto kutokana na vitendo hivyo vya kinyama. Ubakaji ni kosa la jinai ambalo haliwezi kuvimilika na hakuna atakayekwepa sheria kutokana na unyama huo. Mmoja wa wanawake waliobakwa DR Congo anasema:

(SAUTI YA MAMA ALIYEBAKWA)