Skip to main content

Wakimbizi Ivory Coast na Libya wasaidiwe:Jolie

Wakimbizi Ivory Coast na Libya wasaidiwe:Jolie

Balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Angelina Jolie leo ameelezea hofu yake juu ya maelfu ya wakimbizi wanaohitaji msaada wa dharura Ivory Coast na Libya.

Amesema wakati dunia inashuhudia vilio vipya Afrika Magharibi na Afrika Kaskazini ni muhimu kwa pande zote husika kuheshimu haki za binadamu na hasa kwa watu ambao wako kwenye hatari wamekimbia machafuko nchini kwao na wanaoomba hifadhi na kujikuta katika matatizo mapya.

Ametoa wito wa kuwalinda watu hao, kutowalenga wala kuwaumiza. Mapigano mjini Abobo Ivory Coast yamesabisha watoa misaada kushindwa kuwafikia maelfu ya wafuasi wa Alassane Ouattara wakati kwenye mpaka baina ya Libya, Misri na Tunisia maelfu wanasubiri msaada.