Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Somalia iko katika hatihati ya janga la kibinadamu:UM

Somalia iko katika hatihati ya janga la kibinadamu:UM

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Somalia Shamsul Bari leo ameitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza juhudi kushughulikia athari za ukame unaoendelea kuiathiri Somalia na watu wake.

Bwana Bari amesema kiwango cha ukame alichokishuhudia alipozuru nchi hiyo, Kenya na Djiboutti ni cha kutisha na msaada unaotolewa hautoshelezi, watu hawana hudumuma muhimu kama maji ya kunywa, lishe bora na huduma za afya. George Njogopa anaripoti

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Mtaalamu huyo amezitolewa mwito jumuiya za kimataifa ikiwemo Umoja wa Mataifa wenyewe kuongeza bidii ili kutanzua hali mbaya inayoliandama eneo hilo hasa kwa kuzingatia kuwa makundi kama wanawake na watoto ndiyo yako hatarini zaidi.

 

Ameonya na kuonyesha wasiwasi wake juu ya hali mbaya inavyoendelea kumea mizizi na kutaka kitisho cha ukame kama balaa jingine ambalo linaongeza maafa kupindukia yale yalitokana na migogoro ya vita vya muda mrefu.

 

Somalia ambayo kwa miaka mingi imeandamwa na mapigano ya ndani kwa ndani kutokana na kukosekana kwa serikali madhubuti, kwa sasa inaandamwa na majanga mengine ikiwemo la ukame ambalo limesababisha kukoseka kwa chakula cha kutosha. Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 32 ya wakazi wa taifa hilo wapo kwenye hitajio la chakula.