Kiongozi mkuu wa polisi wa Serbia katika Kosovo apatiwa kifungu cha miake 27

24 Februari 2011

Kiongozi mkuu wa zamani wa polisi wa Serbia amehukumiwa kifungo cha miaka 27 jela kwa kuhusika na uhalifu dhidi ya binaadamu na uhalifu wa kivita dhidi ya raia wa Albania wa Kosovo katika mwaka 1999.

Vladiminir Dordevic alikuwa naibu waziri wa Serbia wa mambo ya ndani wakati wa vita vya Kosovo wakati huo.

Mahakama ya kimataifa kuhusu Yugoslavia ya zamani ilioko the Hague ilimkuta Vlastimiri Dordevic na hatia ya kushiriki katika visa vya uhalifu ili kubadili usawa wa kikabila katika Kosovo na kuhakikisha Waserbia ndio wanakuwa wengi na kutawala.

Mahakama ilisema mpango wake ulikuwa ni wa kutekeleza kampeni ya vitisho na maovu dhidi ya Waalbania, kuwahamisha kwa nguvu , mauaji pamoja na kuwanyanyasa.

Mahakama ilimtuhumu Bwana Dordevic kufanya kazi na viongozi wa Jamuhuri ya Yugoslavia akiwemo Rais wake Slobodan Milosevic aliyefariki akiwa korokoroni The Hague mwezi machi mwaka wa 2006 wakati alikuwa akishtakiwa kuhusu uhalifu wa kivita..

Dordevic ni kiongozi mkuu wa zamani Serbia wa nane kushtakiwa kuhusu maovu nchini Kosovo na kiongozi wa sita kuhukumiwa.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter