KM Ban awalaani maharamia wa Somalia

KM Ban awalaani maharamia wa Somalia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema amevunjwa moyo na

kusikitishwa kufuatia ripoti za mauwaji kwa raia wanne wa kimarekani waliotekwa

na maharamia katika pwani ya Somalia.

Duru za vyombo vya habari zimesema kuwa maharamia hao waliwapiga risasi raia hao Wamarekani waliokuwa wakiendesha boti katika eneo la kusini mwa Oman.

Hata hivyo vikosi vya Marekani vinavyofanya doria kwenye eneo hilo vimefanikiwa kuwakamata maharamia 15 na kuwauwa wengine wawili muda mfupi baada ya kufika eneo la tukio.

Akielezea masikitiko yake juu ya kitendo hicho, Ban amesema kuwa mauaji ya waendesha boti hao ni kitendo cha kuogopesha ambacho kinaeleza umuhimu wa kuendelea kuunganisha nguvu za kimataifa ili kuwakabili maharamia hao.