Hali ya hatari yatangazwa New Zealand-OCHA

22 Februari 2011

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA imesema kumetolewa hali ya tahadhari katika eneo la kanisa huko New Zealand kufuatia tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha richter 6.3

Ripoti zilizopo hivi sasa zinasema kuwa watu 65 wamefariki dunia na kuna uwezekano idadi hiyo ikaongezeka kutokana na hali mbaya za majeraha.

 

Kuna uharibifu mkubwa wa mali uliotokea. OCHA kwa kushirikiana wizara ya ulinzi nchini humo inaendelea na operesheni za ukoaji na huduma za kwanza.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter