Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama larefusha muda wa upelekaji vikosi Ivory Coast

Baraza la usalama larefusha muda wa upelekaji vikosi Ivory Coast

Baraza la usalama limereufusha kwa muda wa miezi mitatu mpango wake wa kutuma askari wa kulinda amani kutoka Liberia kwenda nchini Ivory Coast ambako kuna mkwamo wa kisiasa kufuatia uchaguzi wa duru ya pili ya urais wa mwaka uliopita.

Ivory Coast ilitumbukia kwenye mkwamo wa kisiasa disemba mwaka jana wakati rais aliyemaliza muda wake  Laurent Gbagbo alipogomea kuondoka madarakani licha tume ya taifa ya uchaguzi kumtangaza mpinzani wake Ouattara kuwa ndiye mshindi.

Vikosi vya Umoja wa Mataifa vipo nchini Liberia na vingine Ivory Coast vikiendesha opereshini ya amani baada ya eneo hilo la Afrika Magharibi kutumbukia kwenye machafuko tangu mwaka 2002