Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM Ban ataka utumiaji nguvu dhidi ya waandamanaji ukomeshwe mara moja

KM Ban ataka utumiaji nguvu dhidi ya waandamanaji ukomeshwe mara moja

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameyataka mataifa ya Afrika Kaskani na Mashariki ya Kati kujiepusha na matumizi ya nguvu za dola wakati inapojaribu kukabiliana na maandamano ya amani.

Akizungumza katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, Ban amesema amesononeshwa mno na taarifa mbaya zinazotoka huko Bahrain ambako vikosi vya serikali vimepambana na waandamanaji.

(SAUTI YA BAN)

 Pia amewatolea mwito viongozi wa maeneo hayo na duniani kwa ujumla kukaribisha mageuzi.