Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID yaahidi kuongeza mbinu za usalama kwa askari wake Darfur

UNAMID yaahidi kuongeza mbinu za usalama kwa askari wake Darfur

Umoja wa Mataifa umesema kuwa utachukua mbinu za kiusalama zaidi ili kuwalinda askari wake wanaoendesha operesheni za amani katika eneo la Darfur. Pia imesisitiza mpango huo utawafaidia wananchi wa kawaida.

Muungano wa vikosi vya kimataifa vinavyoendesha opereshani zake katika eneo lenye mzozo la Darfur UNAMID huendesha doria zisizo pungua 100 kwa siku, lakini hata hivyo vikosi hivyo hukabiliana na makundi ya wavamizi mara kwa mara.

 

Professor Ibrahim Gambari ni mwakilishi wa vikosi hivyo huko Darfur

(SAUTI YA GAMBARI)