Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yataka kuanzishwa mbinu mpya za kukabili tatizo la umaskini

FAO yataka kuanzishwa mbinu mpya za kukabili tatizo la umaskini

Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO imesema kuwa njia mbadala ambayo ulimwengu unaweza kuepukana na tatizo umaskini ni kuhamisha mpango maalumu ambayo utatilia uzito uzalishaji wa vitu viwili kwa pamoja.

Ripoti hiyo imesema kuwa uzalishaji wa bega kwa bega baina ya chakula na nishati ndiyo mwarubaini kwa kutibu tatizo la njaa ambalo kwa sasa linayaandama mataifa mengi.

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)