Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shughuli za ulinzi wa amani zinataka ushirikiano zaidi- Alain Le Roy

Shughuli za ulinzi wa amani zinataka ushirikiano zaidi- Alain Le Roy

Mashirikiano ya dhati baina ya Umoja wa Mataifa na washirika wake ndiyo nguzo muhimu inayoweza kufanikisha shabaya ya kuwepo kwa shughuli za vikosi vya uletaji amani.

Akizungumza kwenye warsha ya kujadilia changamoto zinazokabili shughuli za uletaji amani, mkuu wa kitengo hicho Alain Le Roy amesema kuwa Umoja wa Mataifa hauwezi kufikia shabaya hiyo pasipo kupata uungwaji mkono toka kwa nchi wanachama wake. Lin Sambili na taarifa kamili.

(SAUTI YA LIN SAMBILI)