Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNEP, Hisense International Co. waanzisha tuzo ya SEED

UNEP, Hisense International Co. waanzisha tuzo ya SEED

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira UNEP limetiliana saini

kuanzishwa kwa tuzo ya ujasiliamali baina yake na kampuni moja ya kimataifa ya

Hisense International Co.

Tuzo hiyo inayojulikana kama SEED Award ni mkakati wa pande zote mbili kuwatambua wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kiwango cha kati namna wanavyoweza kuwa wabunifu kuanzisha miradi ambayo ndani yake inaweka zingatio la mazingira.

Hisense  International ambayo makao yake makuu yako huko China, imesema kuwa  tuzo hiyo ni sehemu ya mchango wa kutambua juhudi zinazofanywa na jumuiya za kimataifa kukabiliana na tatizo la mazingira.

Kwa upande wake UNEP imesema kuwa mshindi wa tuzo hiyo atakuwa mfano wa kuigwa duniani kote hasa kwa kuzingatia kubwa changamoto inayoendelea kuikabili dunia sasa ya uharibifu wa mazingira.