Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya yaanza kutoa chanjo ya Nimonia

Kenya yaanza kutoa chanjo ya Nimonia

Mamia ya watoto nchini Kenya wameanza kupata chanjo ya Nimonia katika wakati

ambapo Umoja wa Mataifa ukiendelea kuendesha kampeni yake ya kutokomeza kabisa

ugonjwa huo ambao unachangia kwa kiasi kikubwa kusababisha vifo vya watoto.

Rais Mwai Kibaki aliungana nakundi la wazazi, wafanyakazi wa wizara ya afya pamoja na mabalozi na wahisani kushuhudia utoaji wa chanjo hiyo kwa watoto ambao ni mpango maalumu wa serikali ulianzishwa kwa ajili ya kutokomeza tatiozo hilo. Alice Kariuki na taarifa kamili

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)