Skip to main content

UNICEF yaahidi kuboresha ushirikiano na wahisani wake

UNICEF yaahidi kuboresha ushirikiano na wahisani wake

Kikao cha bodi ya watendaji wa shirika la umoja wa mataifa linalohusika na watoto UNICEF kimemaliza huku ukitolewa wito kuongezwa kasi ya kuleta mabadiliko na kuongeza mashirikiano zaidi ili kuwafikia makundi ya watoto duniani kote wanaokabiliwa na hali mbaya.

Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimehaidi kuendelea kutoa mafunga ya fedha ili kusukuma mbele miradi ya UNICEF iliyoanishwa kutekelezwa ndani ya mwaka huu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Anthony Lake pamoja na kutoa shukrani zake juu ya misaada hiyo lakini pia amehaidi kuendelea kudumisha mashirikiano kwa shabaya ya kukabili changamoto zinazoendelea kuibuka.