Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghana yageukia nyuklia kuwa na uhakika wa nishati

Ghana yageukia nyuklia kuwa na uhakika wa nishati

Ghana inageukiwa nyuklia katika kutosheleza mahitaji yake ya nishati yaliyosababishwa na ukuaji wa uchumi na kuendelea kwa viwanda.

Hatua hii imekuja wakati nchi hiyo inakabiliwa na ukame na ongezeko kubwa la mafuta yasiyosafishwa.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa taasisiya kitaifa ya utafiti wa nyuklia nchini Ghana Benjamin Yarko kwenye makao makuu ya shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA mjini Vienna.

Bwana Yarko ameshiriki katika mkutano wa wawakilishi kutoka nchi zaidi ya 50 ambao wamekuwa wakibadilishana uzoefu katika kuendeleza na kudhibiti miundombinu ya kitaifa ya nyuklia. Amesema mkutano wao umeangalia tatizo la upungufu wa nishati wakati wa ukame na gharama kubwa za mafuta machafu.

Ameongeza kuwa Ghana ambayo kwa sasa inategemea umeme wa nguvu za maji na gesi imeshuhudia matatizo makubwa ya nishati mara nne kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Ukame unakausha mito na hivyo kutatiza uzalishaji wa umeme.