Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Israel ni lazima isitishe ujenzi wa makazi ya walowezi:Pillay

Israel ni lazima isitishe ujenzi wa makazi ya walowezi:Pillay

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameitaka Israel isitishe ujenzi wa makaazi ya walowezi wa kiyahudi kwenye ardhi ya wapalestina.

Pillay anasema kuwa ujenzi wa makaazi hayo kwenye ardhi iliyotwaliwa ni kinyume na sheria za kimataifa akiongeza kuwa uungwaji mkono wowote ukiwemo misaada ya kujenga makaazi hayo na miundo mbinu yake ni haramu chini ya sheria za kimataifa.

Pillay amesema kuwa siasa za mizozo , amani na usalama vimechangia katika ukiukaji wa sheria za kimataifa zinazolinda haki za binadamu na kuongeza kuwa hakuna mtu yeyote au taifa lolote ambalo linaweza kupendelewa ikiwa limevunja sheria za kimataifa.