Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya Gbagbo yaipiga marufuku Radio ya UM Ivory Coast:

Serikali ya Gbagbo yaipiga marufuku Radio ya UM Ivory Coast:

Wakati huohuo serikali ya Ivory Coast imeipiga marufuku kurusha matangazo radio ya Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast.

Katika taarifa iliyotolewa jana Jumatano kupitia televisheni ya taifa mjini Abijan na viongozi wanaomuunga mkono Rais Laurent Gbagbo imetoa tamko rasmi la kupiga marufuku matangazo ya Radio UNOCI -FM ambayo ni ya Umoja wa Mataifa na ni radio ambayo inasikilizwa sana katika nchi nzima. Radio hiyo imekuwa ikifuatiliwa na serikali ya Ivory Coast tangu kuanza kwa mgogoro wa kisiasa baada ya uchaguzi mkuu mwezi Novemba mwaka jana na kuwekewa vikwazo mbalimbali.

 Hata hivyo licha ya kubanwa radio hiyo imekuwa ikiendelea kurusha matangazo yake kupitia masafa ya 95.3 yasiyo rasmi kama anavyofafanua mkuu wa radio hiyo Sylvain Semilinko.

(SAUTI YA SYLVAIN SEMILINKO)