Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM na wasanii wanatumia muziki kuchagiza afya ya uzazi Tanzania:

UM na wasanii wanatumia muziki kuchagiza afya ya uzazi Tanzania:

Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA limeungana na kundi la wasanii kutoka Marekani na Tanzania kuchagiza kwa njia ya muziki haja ya kuwa na huduma bora za afya ya uzazi katika taifa hilo la Afrika ya Mashariki ambako vifo vya kina mama wakati wa kujifungua ni changamoto kubwa.

Ushirikiano huo umefanikiwa kwa msaada wa mtandao wa kimataifa wa wasanii uitwao MDGFive.com, na umehitimisha warsha ya siku tatu kwa kutoa wimbo maalumu wa kuelimisha zaidi kuhusu tatizo la afya ya uzazi Tanzania. George Njogopa anaripoti.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)