Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yawasaidia Wapakistani wanaokabiliwa na baridi:

UNICEF yawasaidia Wapakistani wanaokabiliwa na baridi:

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linakimbiza misaada muhimu kwa kwa njia ya helkopta kwa maelfu ya Wapakistan walionusurika na mafuriko ambao sasa wako katika hatari kutokana na msimu wa baridi kali.

UNICEF inatoa msaada wa nguo za kujikinga baridi, viatu, mablanketi na vifaa vya watoto wachanga katika maeneo yaliyo kwenye hatari kubwa ikiwemo jimbo la Khyber Pakhtunhkwa ambalo linakabiliwa na theluji Kaskazini mwa Pakistan.

UNICEF pia inasema makambi mengi yanayohifadhi wakimbizi wa ndani waliotokana na mafuriko yatafungwa muda si mrefu kwani serikali inawachagiza kujerea nyumbani katika msimu huu wa baridi. Hata hivyo shirika hilo linasema hali ya kuwataka warejee nyumbani linawatia hofu maelfu ya watu ambao walipoteza kila kitu na hawana mahali pa kwenda.