Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP inaongeza msaada Sri Lanka baada ya athiri za mafuriko

WFP inaongeza msaada Sri Lanka baada ya athiri za mafuriko

Kwa mara ya pili katika kipindi cha chini ya mwezi mmoja mvua kubwa za monsoon zimewalazimisha maelfu ya watu kuzikimbia nyumba zao nchini Sri Lanka baada ya kusababisha mafuriko katika maeneo mengi ya nchi hiyo.

Shirika la mpango wa chakula dunia WFP hiovi sasa linapeleka msaada wa chakula kwa watu laki tano kwenye wilaya zaidi ya 10.

Mkurugenzi mkuu wa WFO Josette Sheeran anasema mafuriko ya Januari yamesababisha athari kubwa kwenye kilimo cha mpungua ambao ndio chakula kikuu cha nchi hiyo jambo ambalo linatishia usalama wa chakula kwa watu ambao wanakabiliwa na matatizo makubwa ya kupoteza nyumba na mali zao. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)