Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa Asia na EU wakutana kujadili mpango wa ajira

Viongozi wa Asia na EU wakutana kujadili mpango wa ajira

Viongozi wa serikali kutoka Umoja wa Ulaya, kundi la wataalamu pamoja na viongozi kutoka Asia wanakutana leo huko Brussels kwa mkuatano wa siku mbili ambao utajikita kujadilia mtizamo halisi juu ya wahamiaji kutoka asia wenye shabaya ya kwenda kufanya kazi barani Ulaya.

Mkutano huo ambao umeandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM utakuwa kama daraja kwa pande zote mbili kufahamishana sera mpya na mtizamo mpya wa usakaji ajira kwa nchi za Ulaya ili kukaribisha majongongeleano na kuondosha sura ya manung'uniko.

Idadi ya wasaka ajira barani ulaya kutoka asia imekuwa ikiongezeka na IOM inakadiria kuwa kiwango hicho kinatazamiwa kukua maradufu hivyo kuna haja ya kutoa elimu na mbinu zitazowafanikisha wasakaji ajira hao