Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Marais watano wa Afrika watumwa kutatua mzozo Ivory Coast

Marais watano wa Afrika watumwa kutatua mzozo Ivory Coast

Marais watano wa nchi za Afrika wakiwemo kutoka Chad, Mauritania, Afrika Kusini, Tanzania na Burkina Faso wako nchini Ivory Coast kutafuta suluhu la mzozo ya uongozi wa nchi hiyo.

Marais hao wametwikwa jukumu la kumuweka madarakani kwa amani Alassane Ouattara akama rais alichaguliwa. Pia wanatarajiwa kuandaa mazungumzo ya ana kwa ana kati ya Laurent Gbabo na Alassane Ouattara. Mzozo wa kisiasa nchini Ivory Coast ulianza kushuhudiwa tarehe 28 mwezi Novemba mwaka ukliopita baaada ya bwana Gbagbo kukataa kuondoka madarakani baada ya kushindwa kwenye uchaguzi huo. Mzozo huo umesababisha vifo vya mamia ya watu huku maelefu ya wengine wakilazimika kuwa wakimbiz ndani na nje ya nchi.