Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka utuklivu kwenye mpaka wa Thailand na Cambodia

Ban ataka utuklivu kwenye mpaka wa Thailand na Cambodia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon ametaka kuwe na utulivu kati ya mpaka wa Thailand na Cambodia baada ya makubiliano ya mara kwa mara kati ya wanajeshi wa nchi hizo.

Kupitia habari iliyotolewa na msemaji wa Ban ni kuwa makabiliano hayo yaliyotokea kati ya tarehe nne na sita mwezi huu yalisababisha vifo vya watu kadha na wengine kuhama makwao na pia kusababisha uharibifu wa mali. Ban ametoa wito kati ya nchi hizo mbili kusitisha makabiliano na kuendelea kutafuta suluhu la kudumu na kuwa na mazunguzmo pamoja na ujirani mwema. Mzozo kati ya nchi hizo mbili ulianza kushuhudiwa mwezi Julai mwaka 2008 kufuatia kuweka wanajeshi karibu na Hekalu la Preah Vihear nchini Cambodia Hekalu lililoorodheshwa kama moja ya maeneo ya kale na shirika la elimu , sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO mapema mwezi huo wa Julai mwaka 2008.