Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asilimia zaidi ya 90 ya mamilioni ya wananchi wa Sudan Kusini wameamua kujitenga na kaskazini:UM

Asilimia zaidi ya 90 ya mamilioni ya wananchi wa Sudan Kusini wameamua kujitenga na kaskazini:UM

Jopo la Umoja wa Mataifa la kuangalia kura ya maoni ya Sudan Kusini leo limekaribisha tangazo la matokeo rasmi ya kura ya maoni ambayo yanaonyesha kwamba asilimia kubwa ya kura zimeunga mkono kujitenga.

Jopo hilo linaamini kwamba matokeo ya kura hiyo ya maoni yanawasilisha matakwa ya watu wa Sudan Kusini na kwamba mchakato mzima ulikuwa huru, wa haki na uliostahili. Flora Nducha na taarifa kamili.