Skip to main content

Tatizo la kimataifa la ukatili wa kimapenzi lazima likomeshwe:UM

Tatizo la kimataifa la ukatili wa kimapenzi lazima likomeshwe:UM

Viongozi wa kisiasa barani Afrika wametakiwa kuongoza juhudi za kukomesha tatizo la kimataifa la ubakaji na ukatili wa kimapenzi dhidi ya wanawake kwenye vita.

Wito huo umetolewa na Margot Wallström, mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili wa kimapenzi kwenye migogoro. Bi Wallström alishiriki katika katika hafla maalumu ya uzunduzi wa kitengo cha wanawake cha Umoja wa Mataifa UN Women mjini Addis Ababa Ethiopia. Bi Mrgot amesema

"Tuko hapa katika tukio hili tukishirikiana na muungano wa Afrika , sio kwa sababu hili ni tatizo la Afrika kama tulivyosikia. Ni tatizo la kimataifa lakini pia katika vita vilivyoko katika bara hili , hili ni suala ambalo tunatakiwa kulikomesha, na linahitaji uongozi wa kisiasa.

Linahitaji ari ya kisiasa na mtazamo mkali wa uongozi kwa sababu ni lazima lianze na viongozi wa kisiasa ambao wanasema hili lazima likome, huu ni uhalifu wa kimataifa. Ni uhalifu sio mila au ngono, ni uhalifu.