Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa UM kuchunguza ukiukaji wa haki Tuniasia

Wataalamu wa UM kuchunguza ukiukaji wa haki Tuniasia

Timu ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa inaanza uchunguzi wa ukiukaji wa haki za binadamu nchini Tunisia.

Ghasia za kupinga serikali ya Tunisia zinaendelea wakati nchi hiyo ikikabiliwa na sintofahamu ya hatma yake.  Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema kwamba ukiukaji wa haki za binadamu ndio kitovu cha matatizo yanayowakabili watu wa Tunisia hii leo.

Timu hiyo ya wataalamu itakutana na uongozi wa mpito, makundi ya jumuiya za kijamii, mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wengine muhimu katika taifa hilo la Afrika Kaskazini.