Skip to main content

Maharamia wa Kisomali wasiruhusiwe kuwepa adhabu:UM

Maharamia wa Kisomali wasiruhusiwe kuwepa adhabu:UM

Kuepuka adhabu kwa maharamia wanaoendesha shughuli zao katika pwani ya Somalia lazima kushughulikiwe kwa kuunga mkono kushitakiwa kwao katika taifa hilo la pembe ya Afrika amesema mshauri wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa.

Bwana Jack Lang ambaye ni mshauri wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kisheria ametoa wito wa kuyasaidia maeneo ya Puntland na Somaliland kuwakamata na kuwashitaki maharamia. Bwana Lang ametaja mapungufu yaliyopo katika juhudi za sasa za kupambana na uharamia pwani ya Somalia na kusema

"Maharamia 9 kati ya 10 wanaokamatwa na inabidi waachiliwe kwa sababu hakuna mataifa yaliyo tayari kuwafungulia kesi, hivyo kuepuka adhabu ni kitu kilichotawala, 9 kati ya 10 wanaokamatwa wanaachiliwa kwa sababu hakuna sheria zilizoandaliwa kuwahukumu.