Skip to main content

Haiti imetakiwa na mkuu wa opereshen za kulinda amani kumaliza mvutano wa kisiasa uliopo

Haiti imetakiwa na mkuu wa opereshen za kulinda amani kumaliza mvutano wa kisiasa uliopo

Haiti imetakiwa na mkuu wa Umoja wa Mataifa wa operesheni za kulinda amani Alain Le Roy kutatua mvutano wa kisiasa uliosababishwa na utata wa matokeo ya uchaguzi wa Rais.

Uchaguzi wa Novemba 28 ulighubikwa na ripoti za udanganyifu na kutokuwa na mpangilio upasao.

Wafuasi wa mwimbaji mashuhuri ambaye ni mgombea Urais Michel Martelly, wamekuwa wakipinga kumuweka mgombea wao katika nafasi ya tatu baada ya mke wa zamani wa Rais Bi Mirlande Manigat na Jude Celestin.

Bwana Le Roy,amelitaka baraza la uchaguzi CEP kutilia maanani mapendekezo ya jumuiya ya muungano wa nchi za Marekani ambayo ni pamoja na kumuweka Bwana Martelly katika nafasi ya pili. Bwana Le Roy amesema

(SAUTI YA ALAIN LE ROY)

Tangu kutangazwa kwa matokeo ya awali ya uchaguzi wa Rais mwezi december mwaka jana, Haiti imeghubikwa na sintofahamu ya kisiasa. Baada ya mwaka mmoja tangu tetemeko la ardhi la Januari 12 mwaka 2010 na ugonjwa wa kipindupindu unaoendelea ni muhimu kumaliza mzozo wa sasa wa kisiasa, ili kwamba serikali na watu wa Haiti wajikite katika changamoto za ujenzi mpya .