Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wawakumbuka waliokufa kwenye tetemeko Haiti

UM wawakumbuka waliokufa kwenye tetemeko Haiti

Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa leo wanawaomboleza watu 220,000 waliokufa katika tetemeko kubwa la ardhi lilotokea katika kisiwa cha Haiti kilioko katika Bahari ya Carribean mwaka mmoja uliopita.

Umoja wa Mataifa ulipoteza wafanyakazi wake wengi kwenye tukio hilo na kufanya tukio la kukumbukwa daima kwani haijapata kutokea kupoteza wafanyakazi wengi kwa wakati mmoja. Jumla ya wafanyakazi 103 walifariki dunia kwenye tetemeko hilo na baadaye wafanyakazi wengine 12 walifariki duniani kutokana na ghasia zilizotokea nchini humo.

Rais wa chama cha wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa Stephen Kisambira amesema kuwa tukio hilo linatia simanzi kwa ulimwengu kwani haijapata kushuhudia idadi kubwa ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakiaga dunia kwa wakati mmoja.

Wengi wa wafanyakazi hao ni wale waliokuwa wakifanya kazi katika kikosi cha kulinda amani na kuleta amani cha Umoja wa Mataifa nchini Haiti MINUSTAH