Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haiti bado inakabiliwa na tishio la kipindupindu:WHO

Haiti bado inakabiliwa na tishio la kipindupindu:WHO

Shirika la afya dunian WHO limesema kuwa wakati Haiti ikiadhimisha mwaka mmoja tangu kutokea kwa tetemeko baya la ardhi, bado nchi hiyo inakabiliwa na kitisho kikubwa cha kipindupindu.

Ripoti zinasema kwamba watu 171,304 tayari wamekumbwa na ugonjwa huo,na waliopoteza maisha wanafikia 3,651. Tetemeko hilo la ardhi lililotokea mwaka mmoja uliopita, lilivuruga mifumo mingi ikiwemo ile ya afya na kupoteza maisha ya wafanyakazi wa afya wanaofikia 300.

Kwa hivi sasa WHO imeanza kuendesha miradi mbalimbali yenye lengo la kuboresha sekta ya afya ikiwa pamoja na kujenga vituo 30 vya afya na utoaji chanjo dhidi ya ugonjwa huo.