Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uzalishaji wa chakula mwaka 2010 uliongezeka kiasi:FAO

Uzalishaji wa chakula mwaka 2010 uliongezeka kiasi:FAO

Shirika la chakula na kilimo FAO limetoa ripoti ya mtazamo wa uzalishaji na bei za chakula kwa mwaka 20010 na kusema uzalishaji uliongezeka kidogo na kufikia tani million zaidi ya milioni 200 , ingawa ulikuwa chini kwa asilimia 1.4 ikilinganishwa na mwaka 2009.

Kupungua kumejitokeza katika nchi nyingi ambazo ni wasafirishaji wakati katika nchi za kipato cha chini na zenye matatizo ya chakula uzalishaji umekadiriwa kuongezeka kwa asilimia 2.5, na ongezeko kubwa linatarajiwa katika kanda zote barani Afrika isipokuwa Afrika Kaskazini.

Bei za vyakula kama mahindi na ngano ilipanda kwa asilimia 50 mwaka jana ikilinganishwa na 2009.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo mtazamo wa mwaka huu wa 2011 unaonyesha kwamba uzalishaji wa baadhi ya mazao utaongezeka ,ingawa uzalishaji wa mazao kama ngano utategemea hali ya hewa katika miezi michache ijayo.

Pia imesema pamoja na kwamba 2010 uzalishaji uliongezeka lakini nchi 29 duniani zinakabiliwa na matatizo ya chakula na zinahitaji msaada kutoka nchi kunusuru maisha ya watu wake.