Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu alaani mauaji ya afisa wa Pakistan

Katibu Mkuu alaani mauaji ya afisa wa Pakistan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mauaji ya gavana wa jimbo la Punjab nchini Pakistan.

Gavana Salman Taseer amepigwa risasi leo Jumanne wakati akipanda gari lake kwenye mtaa wa maduka katika mji mkuu wa Pakistan Islamabad. Katika taarifa yake iliyowasilishwa na msemaji wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemweleze bwana Taseer kama kiongozi muhimu ambaye kifo chake ni pigo kubwa kwa Pakistan.

Ban ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya bwana Taseer, serikali na watu wa Pakistan kwa msiba huo. Imeelezwa kuwa bwana Taseer amepigwa risasi tisa na mmoja wa walinzi wake ambaye hivi sasa anashikiliwa na polisi.