Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM inasaidia wizara ya Afya ya Sri Lanka kudhibiti homa ya kidingapopo

IOM inasaidia wizara ya Afya ya Sri Lanka kudhibiti homa ya kidingapopo

Shirika la kimataifa la uhamiaji linaisaidia wizara ya afya ya Sri Lanka kutoa mafunzo ya afya kwa wauguzi na wahudumu wa afya zaidi ya 100, ya kuhudumia wagonjwa wa homa ya kidingapopo kwenye hospitali kuu ya Vavuniya.

Mafunzo hayo ya maandalizi, umakini hospitali, uwezo wa kuhudumia na njia za kudhibiti yameendeshwa na wataalamu wa magonjwa ya kuambukiza kufuatia mlipuko wa ugonjwa huo nchi nzima mwaka jana. George Njogopa na ripoti kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)