Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhalifu wa mtandao unatoa changamoto katika sheria:EU

Uhalifu wa mtandao unatoa changamoto katika sheria:EU

Dunia hivi sasa imeelezwa kutegemea sana tekinolojia ya mawasiliano na mfumo wa bank umesema muungano wa Ulaya.

Na wakati huohuo biashara haramu ambao wahalifu hupata taarifa, nyezo na utaalamu kwa njia ya mtandao inaimarika.

Muungano wa Ulaya unasema ingawa thamani ya uchumi uliotokana na uhalifu wa mtandao bado haijajulikana,takwimu za karibuni za fedha zilizopotea kutokana na uhalifu huo ni takribani euro bilioni 750 kwa mwaka.

Muuungano huo unasema kiwango cha uhalifu huo ni tatizo kubwa katika utekelezaji wa sheria hasa kukiwa na zaidi ya virusi 150,000 vya computer na namba zingine zinazotumika kwa uhalifu zikiwa katika mzunguko na kutumiwa na compyuta 148,000 kwa siku.

Uhalifu wa mtandao pia umeelezewa kuwa ni mgumu sana kuchunguzwa. Hata hivyo muungano wa Ulaya unasema umeanzisha nyenzo ya kukabiliana na uhalifu huo kwa kutumia kitengo cha uhalifu na upelelezi Europol.

Nyezo hiyo ni pamoja na kuimarisha mfumo wake wa mawasiliano, kuongeza wafanyakazi wenye ujuzi na wataalamu wa masuala ya kompyuta ili kukabiliana na uhalifu huo.