UNDP yapeleka vifaa kusaidia kura ya maoni Sudan Kusini

27 Disemba 2010

Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP limeanza kuwasilisha vifaa kwa ajili ya kufanikisha zoezi la upigaji wa kura za maoni Sudan Kusin.

Masanduko ya kura kwa ajili ya wapiga kura milioni 4 yakiwa na picha aina mbili zinazoonyeshea umuhimu wa zoezi hilo yamewasili tayari katika mji wa Juba. Wananchi wa eneo hilo watapiga kura January 9 mwakani kuamua kama wajitenge toka kwa mamlaka ya Sudan na kujiundia taifa lao ama waendelee kubaki kama ilivyo hivi sasa.

Hapo awali UNDP ilifanikisha zoezi la uandaaji wa vituo vya upigaji kura 3000. Hali ya ulinzi imeimarishwa kwenye eneo hilo, kufuatia mpango maalumu ulioendeshwa na UNDP ambap askari polisi 20,000 walipewa mafunzo maalumu.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter