Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi 14,000 wa Ivory Coast waingia Liberia:UNHCR

Wakimbizi 14,000 wa Ivory Coast waingia Liberia:UNHCR

Zaidi ya wakimbizi 14,000 wamevuka mpaka na kuingia mashariki mwa Liberia kufuatia mzozo wa kisiasa unaoshuhudiwa nchini mwao.

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa inawalazimu wakimbizi hao kutembea kwa masaa au hata siku kadha wakivuka mito midogo inayogawa nchi hizo mbili. UNHCR inasema kuwa kuendelea kuongeza kwa idadi ya wakimbizi hao kumekuwa changamoto kwa wenyeji .

 Wakimbizi hao wanaendelea kukabiliwa na uhaba wa chakula hata baada ya jitihada za serikali na mashirika ya kibinadamu za kugawa chakula. Pia vifo kadha vimeripotiwa miongoni mwa wakimbizi akiwemo mtoto aliyesombwa na maji alipokuwa akivuka mto Cestos. Kwa sasa UNHCR inatoa wito wa kutata raia kupewa usalama na haki ya kutafuta hifadhi.