Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

China kutoa msaada kwa vikosi vya AMISOM

China kutoa msaada kwa vikosi vya AMISOM

Kamishna wa amani na usalama katika muungano wa afrika AU Ramtane Lamamra pamoja na balozi wa china nchini Ethiopia Gu Xiaojie wametia sahihi makubaliono ambapo China itatoa misaada kwa kikosi cha kulinda amani nchini Somalia cha AMISON.

Msaada huo ambao utakuwa wa zaidi ya dola milioni 4 utatumiwa kununua vifaa kwa kikosi hicho cha AMISON. Kutiwa sahihi kwa makubaliano haya kunajiri baada ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuafikia makubalino mwezi huu ambapo katibu mkuu ameomba kuunga mkono kikosi cha AMISON na kuongeza kikosi cha wanajeshi wake hadi wanajeshi 12,000.

Katika azimio hilo baraza la usalama la Umoja wa Mataifa pia limetoa wito kwa nchi wanachama na mashirika ya kimataifa kutoa mchango wa kusaidia kikosi cha AMISON.