Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usafirishaji wa Bidhaa nje kwa Asia-Pacific kukua kwa asilimia 10.5 mwaka 2011

Usafirishaji wa Bidhaa nje kwa Asia-Pacific kukua kwa asilimia 10.5 mwaka 2011

Ripoti mpya iliyotolewa leo na Umoja wa Mataifa inaonyesha kwamba usafirishaji nje wa bidhaa katika Asia na Pacific unakuwa huku viwango vya uchumi vikiongezeka kwa tarakimu mbili kwa mwaka huu wa 2010.

Ripoti hiyo iliyotolewa na kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya uchumi na jamii kwa nchi za Asia na Pacific ESCAP inasema mwaka huu wa 2010 uchumi katika eneo hilo umekuwa na kuongeza usafirishaji kwa asilimia 19.3 na uingizaji bidhaa toka nje asilimia 20.2

Imeongeza kuwa inatarajia kuwa usafirishaji nje wa bidhaa kwa mwaka 2011 utakuwa kwa asilimia 10.5, ukiongozwa na Uchina, India, Uturuki na Malaysia.