Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa kulinda ahaki za watoto wahitimishwa Morocco

Mkutano wa kulinda ahaki za watoto wahitimishwa Morocco

Mkutano wa Jumuiya ya nchi za kiarabu umemalizika huko Marrakesh, Morocco na kupitisha azimio linalozingatia ustawi wa watoto.

Mkutano huo ambao umeratibiwa na Umoja wa Mataifa umetoa mapendekezo ya kulindwa na kuheshimiwa kwa haki za watoto na kusisitiza kuwa nchi zilizoko kwenye jumuiya hiyo ya kiarabu zinapaswa kuhakikisha kwamba zinakomesha tabia ya utumikishaji watoto na kupiga marafuku ndoa za mapema.

Aidha Wajumbe kwenye mkutano huo wameelezea umuhimu wa kupatikana kwa takwimu zinazohusisha harakati za uzuiaji unyanyasaji kwa watoto pamoja na hatua zinazopigwa kukomeshwa kwa hali hiyo.

Ripoti mbalimbali zinaonyesha kwamba maeneo ya mashariki ya kati na kaskazini mwa afrika, ni maeneo ambayo yameshamiri kwa vitendo vya ukatili kwa watoto.